Siku Njema ya-Prof.Walibora nd'o kitabu maarufu katika historia ya Kiswahili kulingana na utafiti.
Riwaya ya Siku Njema, iliyochapishwa mwaka wa 1996 na shirika la uchapishaji Longhorn Publishers PLC yazidi kutamba na kushikilia namba moja kwa umaarufu miaka ishirini baadaye.
Kufuatia utafiti uliofanywa na shirika la Imarisha East Africa Productions Ltd,linalohusiana na masuala yanayofungamana na utafsiri wa lugha ya Kiingereza-Kiswahili,animations,Uchapishaji wa mitandaoni na uandishi wa michezo ya kuigiza, Siku Njema ilivipiku vitabu vingine vilivyowahi kutumiwa shuleni na kuwa maarufu pia.
Kilichoshangaza zaidi ni kung'amua kuwa,hivyo vitabu vilitumika miaka ya juzi kabisa ukilinganisha na riwaya ya Siku Njema.Kawaida, ungetarajia vingeishinda Siku Njema kwa umbali maana vipo freshi kabisa kwenye bongo za wanafunzi na wasomaji lakini ikawa ndivyo sivyo.
Vitabu tulivyoorodhesha vilikuwa vifuatavyo,ingawaje tuliwapa mashabiki wetu nafasi ya kuorodhesha chaguo Lao;
Siku Njema-Prof.Ken Walibora
Utengano-Said A. Mohammed
Chozi La Kheri-Assumpta Matei
Navyo vitabu vilivyoongezwa na shabiki zetu kwenye orodha vikawa; (Pamoja na majina ya waliyoviongeza kwenye orodha);
Harufu ya Mapera-Paul Nganga
Kidagaa Kimemwozea-Teddy Qym
Mhanga nafsi yangu-Dkt.Makhulo wa Makhulo
Nyuma ya Mapazia-Zack Yaona
Pesa Zinanuka-Geoffrey Mosigisi na Baldwin Mwarigha Mwamburi
Dar Es Salaam Usiku
Ukweli ni kwamba,vitabu vyote hivi ni vizuri sana sawa na waandishi wake wamechagia sana katika medani ya Kiswahili.
Hata hivyo,lazima tuwe na kiongozi mmoja kwa wakati.Kwa sasa Siku Njema ya Walibora imeshikilia namba moja na itakuwa hivyo hadi anga ya Kiswahili itakapo kubali hadithi tofauti kuchukua nafasi ya Siku Njema.
Kumhusu mwandishi wa Siku Njema marehemu Prof.Walibora, ni baadhi ya waandishi bora kabisa na waliochangia pakubwa makuzi ya Kiswahili hapa africa mashariki.
Walibora alichapisha zaidi ya vitabu 50.Hadi wakati wa kifo chake cha ghafla alifariki akiwa mwandishi shupavu wa kupigiwa mfano.
Tutaiwakilisha kazi njema aliyoianzisha Prof.Walibora na tutaimarika chini ya kivuli chake.
#Imarisha #ImarishaDigitalReports #SikuNjema.
