top of page
Search

MPE CHOCHOTE LOLANI


Nimetazama LOLANI , Matozi yakanitoka, Nikazivala miwani,. Kwa kiti nikafumka, Kuku ni pake mudzini, sijaamini hakika, MPE CHOCHOTE LOLANI,.Simvishe utalaka,

Alokupa tabasamu,. Si yule tena LOLANI, Malimwengu yamedumu,Na kumuweka chumbani, Mengi yamekuwa sumu,. Na kumtoa kundini, Wala usimhukumu,. MPE CHOCHOTE LOLANI,

Alisimulia vyema,. Makala ya Malimwengu Na kukupeni Huduma,. Mbona alie uchungu, Wakenya wenye huruma,Njooni njo' wanguwangu Simamieni gharama,. Njoni kwa LOLANI KALU,

Mtumeni Mpesa,. Na chote mlichonacho Kimya chenu chamtesa,Msimpe yenu macho, MPE kinamtakasa,. Ajitoe kwa kificho, Tuma japo miatisa,. Kidogo hicho ni kicho.

Walobara na Wapwani,.Kutoa sio ukwasi, Asomjua LOLANI ,. Ajitoe nimuasi, Chochote nyie toeni,. Tusimvishe utasi MPE CHOCHOTE LOLANI,Fanyeni Tena upesi.

@Monscent Namusassi



#Imarisha #Imarishadigitalreports #masaibuyalonani

75 views0 comments

Imarisha East Africa Productions Limited

A Home of Talents
bottom of page