top of page
Search

Imarisha Kiswahili BoreshaTaifa




Umewahi kujiuliza ni wapi tungekuwa bila ya lugha ya kiswahili? Kama jibu lako ni tungekuwa mbele basi jua kwamba wewe unakifukuza kiswahili. Kama jibu lako ni tungekuwa nyuma sana basi jua kwamba wewe unakitukuza kiswahili.

Washairi walitunga mashairi kwa kusifia kiswahili na lugha zote kwa ujumla. Marehemu Prof.Ken Walibora atakumbukwa kwa kauli yake kwamba, 'tusigombanie fito twajenga nyumba moja'' .Na ni kweli kabisa. Ni ukweli mtupu bila lugha tungekwama.

Misahafu inarekodi Mungu Akilalama na kusema kwamba, kama binadamu watakataa katakata kumsifu basi Yeye katika Uungu wake Ataamuru mawe kupata uhai na kuanza kumsifu. Kumekuwa na wazawa wasaliti wa kiafrika ambao wamekidunisha sana kiswahili na kukiona kwamba hakifai. Badala yake wakatukuza lugha za wenyewe ambao hata nao hawajivunii lugha hizo tena. Hamna neno ni haki yao kufanya wapendavyo. Kwenu ndugu zangu kufu langu, Shime na Hongera! Washiriki wote wa Kituo cha Lugha cha Kampamso kongole!! Hamna kundi jingine kama ninyi.

Sisi wapenzi na waenzi wa Kiswahili tukishindwa kupata wafrika ngozi nyeusi kutuunga mkono katika kukipigia debe kiswahili hatutatahayuri katu kwani tayari tumepata mawe ambayo tumeyatia uhai na yatatusaidia kusifu na kukisifia kiswahili. Mawe hayo yanatokea uzunguni kote kule. Wenzetu hao wameamua kuyavulia nguo maji ya kiswahili na hata kuyaoga. Mimi nimeshika dodoki moja nawasugua kwelikweli kwenye uti wao wa mgongo wa lugha ya kiswahili ili wanyoke twaa kama barabara ya kuenda mbinguni.

Hapo nyuma kukatokea tetesi au mzaha wa kiswahili kuzaliwa sehemu fulani kulelewa sehemu fulani vile vile kusikitika kuzikwa tena sehemu fulani.Kuna ukweli upi inaposemwa uwa kiswahili kilizaliwa Kenya,kikalelewa Tanzania kisha kilizikwa Uganda... Hii enzi yetu kiswahili kimebakia kuzaliwa kokote kunako na majaaliwa,kulelewa kuko huko na hata pengine kwingine na kufishwa pia kokote kule.

Kutokana na mitindo mbali mbali inayoibuka kiswahili kimebaki katika mikono mitupu na sote twafahamu kuwa"Mkono mtupu haurambwi". Kiswahili kimebaki kama rehema ya Mungu;kijisambazishe au hata kifie kikiwezekana ambapo najua au tunajua kuwa hapo yote yawezekana.

Tukiangazia nchini Kenya,wakenya wale wa jadi walijivunia kuifanikish lugha lakini sisi wa sasa hakuna cha kujivunia kama si cha kusikitikia. Wakenya hatufai hata tujipige kifua kuwa kiswahili kilizaliwa humu nchini. Sisi tunashuhudia jinsia Lugha yetu inashushwa thamani,inanyanganywa hdhi inayostahili,inatiwa dosari zisizoifaa hata kidogo. Wengi huamini mnyonge hana haki bali mimi nitasema wanyonge hujinyima haki wenyewe.

"Wapenda lugha" huu ndio wakati wa kuzinduka,tujitie mhanga,kufanya chochote kile kinachowezekana na kuamua kuwa lugha yetu ashirafi imestahiki hadhi yake stahili. Ninajua kuwa hili ni janga ambalo wenyewe tumejiingiza na vivyo hivyo tutatanbihi njia wa kujiuzulu kutokana na janga lenyewe.

Cha muhimu ni sisi kuifanya nafsi yetu tukiepnde kiswahili...mara nyingi nafsi tunaichukulia kama kiungo dhahania lakini ni kiungo muhiu sana. Nafsi ni kigezo kikuu katika maamuzi ya kila mwanaadamu. Tuifanye nafsi ipende,tushawishi moyo kuipenda kiswahili kisha sasa tushirikishe viungo vingine aidha kwa kuandika au kimazungumzo au hata kuhifadhi baadhi ya maarifa ya kiswahili.

Hapa sasa kazi ipo,tujibidiishe kukienzi kiswahili haswa enzi hii yetu maongezi yetu yamezoroteja tu tumeegemea tu maandishi bila kujali maongezi yetu. Tujaribu kadri ya uwezo wetu tusiwaruhusu "mawe" waje kutuzungumzia lugha yetu iwe tumeachiwa tu maandishi tuyafanikishe yote.

Nikitamatisha swali kwako;Wewe nawe unafanya nini? Usipojivunia Kiswahili utajivunia nini? Kikwenu ambacho ukikiweka mbele sana mnachinjana kama wanyama? Kazi kwako yangu nayaishilizia hapo. Kumbuka Kiswahili kitukuzwe, kisifukuzwe.

na

Sumaiyah saleh

Mwanafunzi-Mt.Kemya University.

57 views0 comments

Imarisha East Africa Productions Limited

A Home of Talents
bottom of page