top of page
Search

Chanzo Cha Mimba za mapema kipindi Hiki Cha Korona nchini Kenya


Kulingana na takwimu ambazo zimekuwa zikitangazwa na wizara ya afya ni wazi kuwa tangu watoto wa kike warudi nyumbani kwa sababu ya kuzuia kusambaa zaidi kwa homa hii ya korona, wengi wao tayari washaringwa mimba ambazo wazazi hawakuzitarajia wala watoto wenyewe kuzitarajia.

Imewekwa wazi kuwa wengi wa wanafunzi hawa ni wenye umri Kati ya miaka kumi na minne na kumi na tisa wamepachikwa mimba na jamaa zao ; wajomba, Kaka ,baba miongoni mwa wengine. Jambo hili Lina mengi ya kutufunza sisi ambao bado hatujanaswa kwenye mtego huo. Ingawa haya yote yanajiri Ni wazi kuwa:

Wazazi wamelegeza kamba katika malezi ya watoto wao. Wamewatelekezea walimu majukumu zaidi na kusahau kuwa wana mchango ambao wanafaa kutoa katika malezi ya wanawao.

Fauka ya hayo, imedhihirika wazi kuwa mwalimu ni mlezi mwema zaidi, ingawa wengi hawakubaliani na hili, nadhani kutokana na hali ilivyo sasa hili linasadifu!

wazazi wengi hawawapi wana wao mafunzo kuhusiana na suala la tendo la ngono. Idadi kubwa ya wazazi wanaamini kuwa kuzungumza na wana wao kuhusiana na Jambo hili ni ukosefu wa heshima ni aibu. Wahenga walisema kuwa usipoziba ufa utajenga ukuta . Iwapo wazazi watajitahidi kuzungumzia jambo hili na watoto wao; wa kiume na wakike ambao wanabaleghe mustakabali mwema . Watoto hawa wanahitaji kuelezwa athari ya kujihusisha na ngono za mapema.

Aidha, wanafaa kuelezwa jinsi matumizi ya dawa za kulevya yanaweza kuathiri maisha yao. isitoshe, watoto ambao wamehitimu miaka kumi na minne wanafaa kujuzwa kuhusiana na matumizi ya mipira ya kondomu. Wapo wazazi ambao husema kuwa kuwapa watoto mafunzo haya Ni kuwapotosha Ila wanajaribu kufumba macho kuwa watoto hawa hushiriki vitendo vya mapenzi mpaka pale wanapomeza haragwe.

Mwisho tuwe karibu na mabinti zetu ili kuwapa mawaidha kuhusiana na jinsi ya kupambana na uchu wa mapenzi kwa njia sahihi . Pia tuwafunze kuvaa kistaarabu na kuwakinga kutokana na Yale yanayoweza kuwatia majaribuni. Tuwe nyuma yao na kumulika nyayo zao vizuri

Endapo tutazingatia haya yote tutaweza kukomesha mimba za mapema na hata uavyaji mimba baina ya mabinti zetu. Hili litasaidia kujenga jamii yenye ustaarabu na wastaarabu ndani yake


ONGWAE BRIDGIT KWAMBOKA

Chuo Kikuu cha Kenyatta.

#Imarisha #Imarishadigitalreports #mimbazamapema


82 views0 comments

Recent Posts

See All

Imarisha East Africa Productions Limited

A Home of Talents
bottom of page